WALE WA PESA MBOVU WABURUTWA MAHAKAMANI "WANANE WATUMISHI BoT, HASARA BIL.4"

3 Просмотры
Издатель
Watu 13 wakiwemo watumishi wananane wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka 6 ikiwemo kuharibu noti za 460,000 za Elfu 10 na kuisabbaishia benki hiyo hasara ya zaidi ya


Watumishi hao wa BoT ni Mariagoretha Kuzugala, Henry Mbowe, Asha Sekiboko, Cecilia Mpande, Agripina Komba, Zubeda Mjewa, Khadija Kassunsumo na Mwanakheir Omary. 

Washitakiwa wengine ni Alistides Genand, Shukuru Mchegage, Musa Chengula, Zaituni Chihipo na Respicius Ishengoma ambao walisomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Godfrey Isaya. 

Kwa pamoja washitakiwa hao ambao wamekosa dhamana katika kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi namba 100 wamesomewa mashitaka yao na jopo la mawakili wanne wa Serikali likiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi.

Inadaiwa kuwa kati ya Januari mwaka 2017 hadi Septemba 30 mwaka 2019, watumishi hao wa BoT kwa kuvunja majukumu yao ya kazi waliwezesha utendekaji wa kosa la kuongoza genge la uhalifu. 

Mawakili hao wa serikali waliendelea kudai kuwa, katika tarehe na maeneo hayo, jijini Dar es Salaam, kwa mawasilisho ya kilaghai, kwa kujua na kwa mpango wa kitapeli washitakiwa wote walijipatia faida ya kutoka BoT baada ya kuwasilisha noti hizo ili zibadilishwe.
Категория
Фантастика онлайн
Комментариев нет.
Яндекс.Метрика